|
|
|
![]() ![]() |
||
|
Gazeti la INJILI Kwenye Internet http://munishi.netfirms.com Tel. 254722602445 E-mail:fmunishi@hotmail.com Or munishifaustin@yahoo.com "Nyakati" liko njia panda Gazeti huru la kikristo "Nyakati" liko njia panda, baada ya gazeti la "Njia" kuingia kwa kishindo katika masoko ya kusambaza magazeti Tanzania. "Nyakati" ambalo ni changa kiusajili lakini kongwe kiutendaji, Lilianza kwa kasi ya kutisha, mpaka washindani wao " MsemaKweli" wakaonekana kusalimu amri. Nalo gazeti jipya kiutendaji lakini kongwe kiusajili "Njia" limetinga uwanjani, na kuwafanya "Nyakati" kuwa njia panda. Idadi ya magazeti imeongezeka, wakati soko ni moja. Sasa itategemea akili kichwani mwao. Kuna fununu kwamba "Njia" kiusajili mhariri wake mkuu ni Arnold Victor Msuya wakati "Nyakati " nao mhariri wao mkuu ni huyo huyo arnold Victor Msuya. Sijui kama nao "MsemaKweli wamefuta jina la mhariri huyo kwa msajili, Lakini hata hilo mhariri wake mkuu alikuwa Bwana Msuya. Kile "Nyakati walichowafanyia "MsemaKweli.", Yaani kumchukua mhariri mkuu, wanaweza wakafanyiwa yayo hayo na gazeti la "Njia". Waswahili wana msemo usemao kwamba "Mwosha Huoshwa", Kwa maana ya mtenda naye hutendewa. Wengi wanasubiri waone kama wafanyikazi wa "Nyakati" watahamia "Njia". Hilo likifanyika, msemo kwamba mtenda hutendewa utakuwa umetimia. Katika gazeti la "Nyakati", Kuanzia mhariri mkuu, Meneja matangazo na baadhi ya waandishi walitoka kwenye gazeti la "MsemaKweli". Ndio kwanza "Nyakati" lilikuwa linakita mizizi chini liweze angalau kuwalipa wafanyikazi wake ambao wengi wanafanya kazi kwa misingi ya kujitolea. Hiyo inaeleweka. Gazeti la kidini ambalo halina wafadhili, Tena halifungamani na kanisa lolote, Kufika hapo lilipofika linastahili kupongezwa. Lakini ni vizuri kupokea michango, huku wakiwa macho michango hiyo isiwaondolee uhuru wao wa kuandika ukweli. Wachunguzi wa MEDIA za kidini wanadokeza kwamba sasa kutakuwepo na ushindani mkubwa katika magazeti haya matatu. Kuanzia kunyanganyana wafanyikazi, Matangazo, Na ikididi hata habari watakuwa wakizigombea. Mradi washindane kitaaluma na kiroho, Tanzania inaingia ukurasa mpya wa Media za kidini. Tunayatakia magazeti yote matatu kila la Kheri katika kuieneza Injili kwa njia ya magazeti. Wakumbuke tu kwamba vita vyetu si juu ya damu na nyama. Kwa wasomaji, Sasa wategemee habari zilizofanyiwa utafiti wa kutosha. Kwa watangazaji nao wategemee matangazo yanayoheshimu makubaliano ya awali. Kama tangazo lilikuwa robo ukurasa na makubaliano yakawa yalikuwa hivyo, sasa hakuna sababu ya kukubali chochote nje ya makubaliano. Tangazo likikosewa ni mawili. Aidha walisahihishe na kulirudia, La sivyo warudishe pesa na mtangazaji awe huru kutangaza kwingineko. Magazeti ya kidini yanapokuwa mengi ni baraka ya kumfanya mteja awe mfalme. Mimi mwenyewe ni mfano ulio hai. Niliwapa "Nyakati" Tangazo, tukakubaliana bei na ukubwa wa tangazo, waliyonifanyia baadaye sitosahau.
Mara nyingi watu husema kwamba, Ukitaka ufanyiwe kazi yako vizuri, usiwape watu waliookoka kazi hiyo. Binafsi siamini hivyo. Lakini gazeti la Nyakati wananishawishi niamini hivyo. Usifikiri kwamba ninawakosoa, Hapana. Siwezi kufanya hivyo. Lakini niliwapa TANGAZO waliweke kwenye ukurasa wa mbele wa Nyakati toleo91. Tulikubaliana bei na nikawalipa. Tukakubaliana ukubwa wa tangazo, Isitoshe nikalibuni tangazo lenyewe na kumpatia meneja matangazo. Tulikubaliana litoke lilivyo. Lilipotoka siyo tu lilikuwa tofauti, Bali lilikuwa dogo kwa ukubwa tuliokubaliana, Mbaya zaidi hata maandishi waliyabadili. Nilipompigia simu meneja matangazo kulalamika, Yeye alicheka saaana na kusema Bwana Yesu asifiwe. Kweli Yesu atasifiwa wakati mimi nalia moyoni? Ndiyo maandiko yanasema tushukuru katika kila jambo. Ikiwa maana ya maandiko hayo ni hii basi wakristo tutajiepusha kufanya biashara na ndugu zetu wakristo ili kuepuka makwazo. Ikiwa tutatumia andiko kwamba ndugu yako sharti akukosee mara saba mara sabini, Je 'Nyakati' wamebakiza kunikosea mara ngapi ndio nilalamike? Hapana siwachukii 'Nyakati'. Ndiyo maana nasema yaliyo moyoni mwangu. Wakiona vyema warekebishe na waliweke tangazo kama tulivyokubaliana, Wakiona ndio nimeliwa hivyo, Basi nitafanyaje? Nitawaombea Mungu awaongezee hekima ya kufanya biashara ya gazeti KIROHO na kitaaluma kuliko kuifanya kiroho tu. Makwazo hayana budi kuja, Lakini ole wake yule ambaye yaja kwa ajili yake. Meneja matangazo upooo??? Najua utacheka sana kama kawaida yako. Jamani mnaonaje? Ni haki mzee Mwangomola KIDEVUU aendelee kucheka wakati mimi nalia? Msifikiri nagombana na 'Nyakati' kama gazeti, lakini mtani wangu Mwangomola amezidi. Lazima nimpashe ukweli wake. Najua atakuja Nairobi karibuni. Je nilipize jino kwa jino? Hapana siwezi kufanya hivyo. Nitatumia andiko lisemalo ADUI YAKO MPENDE. Akija safari hii nitampekeka hoteli kubwa zaidi ya ile aliyolala akichukua tangazo. Alikula Githeri yaani maharage na mahindi wakati ule, Akija sasa baada ya kunikosea atakula kuku na chipsi. Na yote hayo ni kumpalia makaa ya moto kichwani. Angalieni tangazo lenyewe hapo juu muone jinsi Nyakati walivyonifanyia. Tangazo dogo lenye rangi ya nyano ndilo walilochapisha kinyume na lile langu nililobuni mwenyewe. Badala ya http://munishi.netfirms.com wao wameandika Http:// munishi.netfirms.com Kwenye internet ukiweka SPACE mahali ambapo hakuna basi ukurasa husika hauwezi kufunguka. Pia ukiweka herufi kubwa mahali pa herufi ndogo, Web Site haiwezi kufunguka. Kwa kuwa tangazo lilimaanisha kuitangaza web site, Lengo zima limeharibiwa na makosa hayo. Sasa hivi kuna watu wanaojaribu kuifungua web site yangu na hawawezi kufanya hivyo. Wengi wameniandikia kuniita muongo lakini Meneja matangazo wa Nyakati yeye anacheka saaaana. Mungu ambariki. Amwongezee weupe kwenye meno yake ili acheka na kucheka halafu acheke tena. Mimi nilie tu nicheke nina mbavu??? |
||||||||||||
|
|
|
|