Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la NYAKATI
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Gazeti la Nyakati
Kwenye Internet

http://nyakati.netfirms.com

Tel. 255744267987 E-mail:
nyakati@yahoo.com

Mwanzilishi wa Kenya studio akumbukwa.

Marehemu John Mwangi Mwariri.

Mzee wetu ametuacha. Anakumbukwa na wote alioishi nao kwa amani na upendo. Imani yake haikuwa maneno matupu, bali iliambatana na matendo mema. Injili siyo maneno matupu. Ni nguvu na uweza ambao unajidhihirisha katika matendo yake. Mtu akiiamini Injili, Maisha yake hayawezi kubaki yalivyokuwa kabla ya kuiamini Injili.Atabadilika. Maneno na matendo yake yataonyesha matunda ya Injili. Yale unayoyaamini halafu ukayasema, lazima yafanane na matendo yako. Kuamini na kusema pekee hakutoshi.

Tuombe

Ee Mungu Baba. Tunakuja kwako kwa jina la mwanao Yesu Kristo. Sisi ni wanadamu wenye mapungufu mengi. Kati yetu kuna watu waliovaa mavazi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu wakali. Tayari wameanza kuliumiza kanisa lako. Tunawaleta kwako tukiwaombea mioyo yao ibadilike. Tunawapenda, Ni ndugu zetu. Tusaidie tuweze kuwa wazi mmoja kwa mwingine ili tuweze kuonyana na kujengana kiroho. Ukuta uliojengeka kati yetu na kuwafanya wayafiche yasiyofichika kwako tunakuomba uubomoe. Walo dhaifu wawe huru kuonyesha udhaifu wao, ili wasaidiwe katika upendo. Hatuwezi kuwa na mapungufu yanayofanana kwa wakati mmoja, Ndiyo maana neno lako haliwezi kumezwa na udhaifu wetu wanadamu. Wewe ni mkamilifu nasi tunaokuamini na kutegemea nguvu zako, Utatukamilisha tuwefanane nawe. Roho wako wa upendo alitawale kanisa lako ili yakiwemo maonyo yatolewe kwa lengo la kulijenga kanisa na siyo kulibomoa. Watumishi wako tujalie neema yako. Tuweze kuliongoza kanisa lako kama ambavyo ungefanya mwenyewe.

Siyo tujionyeshe kwamba sisi ni bora kuliko wengine, Bali uwezo wako utunyenyekeze kuwatumikia walio chini yetu. Ulimtuma Yesu aje atumike duniani, Isitoshe akafa kwa ajili ya dhambi zetu, Watumishi wako tufundishe siri ya kutumika na siyo kutumikiwa. Umasema tujihadhari na manabii wa uongo. Tupe hekima na utambuzi wa kuzitambua roho zinazojiingiza kwa siri kanisani ili kuliharibu kanisa lako. Bwana mwenye rehema na upendo mwingi wa ajabu. Wasamehe wote waliolisikia neno lako leo na kuamua kuyabadili matendo na maisha yao. Wanapoamua kukurudia wewe usiwatupe nje. Hawana mwingine ila wewe. Wakumbatie tena kwa mikono yako, wazione rehema na nguvu zako ziponyazo magonjwa yote . Hata kama adui alipata nafasi ya kuwashambulia kwa magonjwa na matatizo mbali mbali walipokuwa mbali nawe, Sasa wamerudi ili uwaondolee yote mabaya maishani mwao. Waondolee magonjwa miilini mwao, Na badala yake wape afya njema. Waponye Bwana. Waondolee huzuni maishani na badala yake uwape furaha ya ajabu maishani. Wanaoomboleza wape sababu ya ya kuwa na tumaini jema maishani. Tumeomba machache hayo tukiamini kwamba umetusikia na kutujibu, Kwani tumeomba katika jina lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu. Amen.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi

 
| http://munishi.netfirms.com |